MAONESHO YA 23 YA NANENANE NA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA
Maoesho ya kilimo Nanenane kwa kanda ya nyanda za juu kusini yameingia
siku ya nne huku banda la Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda likionesha
kuwa na mvuto wa hali ya juu kuwafanya wananchi wengi kuvutika kuja
kutembelea na kujifunza mambo yanayopatikana katika Halmashauri hiyo.
Moja ya kivutio kikubwa ni kutangaza eneo la uwekezaji la Luhafwe kama
ilivyo sera ya nchi ya Viwanda ili kukuza uchumi na kuwaletea wananchi
maisha mazuri kwa kutumia kilimo chenye tija. Pichani ni Afisa wa
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda akitoa maelezo na elimu ya ramani ya
eneo la uwekezaji la Luhafwe kwa wananchi waliopata fursa ya kutembelea
banda la Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda akiwemo na Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya Mpanda Romuli Rojas John
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda
amepongeza kwa dhati kazi nzuri inayofanyika na kuwatia moyo wananchi
wa wilaya ya Tanganyika kutokana na juhudi kubwa ya kuleta maendeleo
kupitia shughuli za uzalishaji hasa kilimo kwa kuwa ndiyo uti wa mgongo
kwa taifa, Pia akaahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu katika
kusukuma kilimo kwenye Halmashauri yake kwa kushirikiana na wadau
wengine wa maendeeo na kusisitiza wawekezaji kuja kuwekeza kwenye
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kupitia maonesho hayo wanakaribishwa.
No comments:
Post a Comment