Wednesday 23 May 2018

Halmashauri ya wilaya ya Mpanda imekabidhiwa magari 2 na kumpyuta 25 kutoka serikali Kuu.

Halmashauri ya wilaya ya Mpanda imekabidhiwa magari 2 na kumpyuta 25 kutoka serikali Kuu. Vitendea kazi hivyo vimekabidhiwa na mbunge wa Mpanda vijijini mhe. Moshi Kakoso Mei 19, 2018 katika viwanja vya shule ya msingi Mpandandogo.
Gari moja aina ya ‘Toyota landcruiser-picup’ iliyotolewa na wizara ya maliasili na utalii kwa lengo la kulinda misitu na vyanzo vya maji katika Halmashauri ya wilaya ya Mpanda. Gari nyingine ni la kubebea wagonjwa lililotolewa na wizara ya afya, wazee, jinsia na watoto.
Hata hivyo katika hafla hiyo, Mkuu wa uendeshaji mfuko wa mawasiliano kwa wote(UCSAF) mhandisi Albert Richard amekabidi kompyuta 25 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda zenye thamani ya shilingi milioni 50. Baada ya kupokea kompyuta hizo zikakabidhiwa kwa wakuu wa shule za sekondari na moja kwenda kituo cha polisi Mishamo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Romuli Rojas John alishukuru kwa kupata magari hayo 2 na kompyuta 25. Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ina eneo kubwa kiutawala na maeneo mengi hayafikiki kiurahisi, kunahitajika magari mapya na yenye uwezo wa kuhimili changamoto za barabara zetu.
“Kwa mkoa wa Katavi, Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ndiyo halmashauri yenye eneo kubwa kuliko Halmashauri zingine. Nusu ya eneo la Halmashauri ni misitu tengefu na ushoroba. Nina watendaji vijana na wasomi wenyeuwezo wa kutunza vizuri vitendea kazi hivi.” Alisema Romuli
Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ina magari mengi makukuu na baadhi yameegeshwa kutokana na kuhitaji matengenezo makubwa na kwa gharama kubwa. Kwa mwaka wa fedha 2017/2018 tumepata magari mapya 3.


Mbunge wa Mpanda vijijini mhe. Moshi Kakoso(wa kwanza kutoka kulia) amepokea kompyuta 25 zenye thamani ya mil. 50 kutoka mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF).

Mbunge wa Mpanda vijijini mhe. Moshi Kakoso(wa kwanza kutoka kulia) amepokea kompyuta 25 zenye thamani ya mil. 50 kutoka mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF). Akikabidhi kompyuta hizo, Mhandisi Albert Richard amesema kuwa kompyuta hizo zitasaidia kuinua taaluma ya wanafunzi wa shule za sekondari zilizopo katika Halmashauri ya wilaya ya Mpanda.



Mkurugenzi Mpanda DC akabidhiwa magari 2

Mkurugenzi Mpanda DC akabidhiwa magari 2
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda, Romuli Rojas John ( wa kwanza kutoka kushoto) amekabidhiwa funguo za magari mawili kutoka kwa Mbunge wa Mpanda vijijini mhe. Moshi Kakoso. Magari hayo yametolewa na serikali kuu kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi katika Halmashauri ya wilaya ya Mpanda.


Wajumbe wa kamati ya afya Mwese wamejipanga kukamilisha ujenzi

Wajumbe wa kamati ya afya Mwese
Wajumbe wa kamati ya afya Mwese wamejipanga kukamilisha ujenzi na ukarabati wa kituo cha afya kwa wakati. Hayo yalisemwa mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wakati wa ziara ya kikazi iliyofanyika Mei 18, 2018.


Serikali yatoa Mil. 900 vituo vya afya Mwese, Mishamo

Serikali yatoa Mil. 900 vituo vya afya Mwese, Mishamo

Serikali ya awamu ya 5 imeleta neema ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya vya Mishamo na Mwese. Kituo cha afya cha Mishamo kimepata milioni 400 za kujenga wodi ya kina mama, chumba cha kuhifadhia maiti, maabara, sehemu ya kuchomea taka ngumu na miundombinu mingine inayohusiana na afya.
Ujenzi wa kituo hicho unaenda vizuri na sasa umefikia katika hatua za umaliziaji. Wananchi wamejitoa sana katika kusomba mawe na matofali.
Wakati kituo cha afya cha Mwese kimepata shilingi milioni 500 na tayari zimeshaingia katika akaunti ya kijiji tangu Mei 9, 2018. Wananchi wa kata ya Mwese wameshaweka mikakati ya kuhakikisha ujenzi na ukarabati wa nyumba 9 za wahudumu wa afya zinakamilika mapema.


Friday 11 May 2018

SHAMRASHAMRA ZA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU WILAYA YA TANGANYIKA 04/05/2018 YAVUNJA REKODI
Mwenge wa uhuru umewasili Wilaya ya Tanganyika tarehe 04/05/2018i kwa ajili ya uzinduzi wa miradi mbalimbali ya Maendeleo