Friday 1 June 2018

A default home page
MPANDADC.GO.TZ

Serikali imetoa milioni 500 kwa kazi hiyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Bw. Hamadi Mapengo (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na baadhi ya madiwani na watalaam pamoja na wajumbe wa kamati ya afya Mwese wakiangalia eneo linalotarajiwa kujengwa majengo mapya ya kituo cha Afya cha Mwese. Serikali imetoa milioni 500 kwa kazi hiyo.



Viongozi Wakuu wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda wakiteta jambo kabla ya kuanza kikao cha baraza maalum

Viongozi Wakuu wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda wakiteta jambo kabla ya kuanza kikao cha baraza maalum. Baraza hilo limefanyika Mei 29, 2018 katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa halmashauri mhe. Hamadi Mapengo, Mkurugenzi Mtendaji Romuli John, Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mhe. Salehe Mhando, mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanganyika mhe. Yassin Kibiriti na makamu mwenyekiti mhe. Theodora Kisesa.



Wahudumu wa afya ya msingi wa kutoka Halmashauri ya wilaya ya Mpanda na Nsimbo wakipatiwa mafunzo

Wahudumu wa afya ya msingi wa kutoka Halmashauri ya wilaya ya Mpanda na Nsimbo wakipatiwa mafunzo katika ukumbi wa Lyamba.Mafunzo hayo yameendeshwa na waratibu wa huduma ya mama na mtoto kwa kufadhiliwa na taasisi ya Jane Goodall (JGI).




Madiwani wakifurahia jambo la maendeleo katika kikao cha baraza maalum

Madiwani wakifurahia jambo la maendeleo katika kikao cha baraza maalum. Baraza hilo limefanyika Mei 29, 2018 na lilifadhiliwa na taasisi ya Jane Goodall (JGI)



Mkurugenzi wa taasisi ya Jane Goodall Bw. Emmanuel Mtiti akiwashukuru wajumbe wa CMT ya Halmashauri ya Mpanda (hawapo pichani). Watumishi wamejengewa uwezo wa kufanya kazi kwa kushirikiana kwa kila idara ili kuweza kutekeleza lengo la kupunguza ongezeko la watu na kufanikisha utunzaji wa mazingira.


Wajumbe wa CMT wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mafunzo ya kikao kazi

Wajumbe wa CMT wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mafunzo ya kikao kazi cha namna ya kufanya kazi kwa kushirikiana kwa pamoja. Kikao hicho kimeendeshwa na taasisi ya Jane Goodall (JGI) katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda, Mei 30, 2018. Wa tatu kutoka kulia (mstari wa mbele) ni Bi. Phoebe Samwel kutoka JGI.



SASA HIVI MOTO UNAENDELEA KUWAKA KATIKA MLIMA WA LIYAMBAMFIPA ULIOKO ENEO LA KATA YA KAREMA UNAWAKA MOTO BAADA YA KUWASHWA NA WATU WASIOFAHAMIKA NA ENEO LILILOZUNGUKA MLIMA HUO KUNA MAKAZI YA WATU. BAADHI YA WANAKIJIJI WAMEFANIKISHA KUJIKINGA NA MOTO HUO KWAKUKAA PEMBEZONI MWA NYUMBA ZAO WAKIJARIBU KUUZIMA MOTO HUO KWA MATAWI MABICHI USIJE ZURU NYUMBA ZAO.
MWASLI LANGU JE MOTO HUU UNGEWAKA USIKU NANI ANGEJUA NA KUPAMBANA NAO?