Friday 1 February 2019

HALMASHAURI YA WILAYA YA MPNDA YAJIPANGA KIKAMILIFU KUIMARISHA MBINU ZA UFUNDISHAJI MASHULENI.

HALMASHAURI YA WILAYA YA MPNDA YAJIPANGA KIKAMILIFU KUIMARISHA MBINU ZA UFUNDISHAJI MASHULENI.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda (wa kwanza kutoka kulia) akiongozana na afisa elimu msingi Bw. Kenny Shilumba na sisita Rose Sungura wakiangalia zana za kufundishia wanafunzi wa awali na darasa la kwanza. Mafunzo hayo yameratibiwa na OR-TAMISEMI kwa kushirikiana EQUIP- Tanzania. Jumla ya walimu 82 na maafisa elimu wa kata 13 wamepatiwa mafunzo ya namna ya kuinua elimu katika wilaya ya Tanganyika.

NIMWENDO WA JET KWENYE UJENZI WA MADARASA

HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA NIMWENDO WA JET KWENYE UJENZI WA MADARASA
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Bw. Romuli Rojas John (wa kwanza kutoka kulia) akiwa na afisa mipango Bw. Dotto Kwigena na Afisa elimu sekondari Bw. Michael Lyambilo, wakiteta jambo katika eneo la ujenzi wa sekondari Sibwesa. Siku hiyo uongozi wa mkoa wa Katavi na wilaya ya Tanganyika walifika kuona hatua ya ujenzi wa shule mpya ili ziweze kufunguliwa na kuchukua wanafunzi 2019.

HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA YA JIPANGA KIKAMILIFU JUU YA DARASA LA AWALI

HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA YA JIPANGA KIKAMILIFU JUU YA DARASA LA AWALI

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Bw. Romuli Rojas John (wa kwanza kutoka kulia) akiangalia moja ya zana ya ufundishaji iliyotengenezwa na mwali wa darasa la kwanza. Zana hiyo imetengenezwa kwa kutumia mmea wa upupu pamoja na karatasi ya manila

 

MPAKA KIELEWEKE

HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA YA JIPANGA KIKAMILIFU JUU YA DARASA LA AWALI "MPAKA KIELEWEKE"
Hiki ni mfano wa kitanda kilichoandaliwa na mwalimu wa madarasa ya awali na kwanza kwa ajili ya kufundishia watoto namna ya kuandaa kitanda kabla ya kulala. Mambo kama haya yanasaidia kuwafundisha watoto wawe nadhifu na kutunza miili yao na kuwa safi muda wote. Mafunzo hayo yamefanyika Januari 28, 2019 katika ukumbi wa shule ya Mt. Maria-Mpanda.


Bw. Amosi Makala atiatimu Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda

Mkuu wa mkoa wa Katavi Bw. Amosi Makalla (wa pili kutoka kushoto) amefanya ziara ya kutembelea shule za sekondari zinazotarajia kuchukua wanafunzi waliofauli na kukosa nafasi. Wilayani Tanganyika kuna wanafunzi 363 na wanatarajia kujiunga kidato cha kwanza 2019 katika shule za Sibwesa, Bulamata na Ilangu.