Friday 14 December 2018

ZAIDI YA NYUMBA KUMI ZIMEATHIRIKA KUTOKANA NA MVUA


ZAIDI YA NYUMBA KUMI ZIMEATHIRIKA KUTOKANA NA MVUA

Zaidi ya nyumba kumi zimeathirika kutokana na mvua iliyonyesha juzi ikiwa imeambatana na upepo mkali katika kijiji cha kabungu Kata ya Kabungu Wilaya ya Tanganyika na kusabaisha familia nane kukosa makazi na kuhifadhiwa na wasamalia wema.


Akitoa taarifa  ya athari za mvua hiyo mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya iliyoongoza na kamati kamati ya maafa Afisa taarafa wa Tarafa ya Kabungu Odes Gwamaka ameleza kuwa baada ya kupokea taarifa hizo uongozi wa serikali ya kijiji kata na Tarafa walifika eneo la tukio kuwajulia hali wahanga na  kuchukua hatua za haraka kuwapa msaada wa kibinadamu ikiwa ni pamoja na kuwatafutia mahali pa kulala kwa wale walioezuliwa nyumba zao.
 Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama na kamati ya maafa ya wilaya ametembelea  wahanga na kuwapa pole na msaada ya awali ya kibinadamu kama chakula,na kutoa maaelekzeo tathimini ifanyike mapema ili kujua hasara iliyopatikana 

Aidha amewaelekeza wananchi wanapojenga nyumba waepuke ile tabia iliyozoelekea ya kutokufunga lenta ,kwani nyumba yenye lenta inakuwa imara Zaidi,na kusisitiza kupanda miti kwenye maeneo yao kwa kuwa inasaidia kupunguza kasi ya upepo  pindi mvua zinaponyesha zhasa zile za upepo mkali.   

 Kwa Upande wake Katibu wa Kamati ya maafa ya  wilaya ya Tanganyika Reginald Mhango ambaye pia ni Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya  kwa kushirikiana na uongozi wa Kijiji ,Kata  na Tarafa  ametoa mchanganua wa msaada uliopatikana  na jinsi utukagawiwa kwa walengwa,ambapo kwa harakahara vitu vilivyolewa unga wa sembe,maharage,sabuni sukari vinathamani ya Zaidi ya shilingi laki tano kwa kuthamanisha.

Diwani wa Kata ya Kabungu Christina Reonard Sanane ameshukuru kwa niaba ya wananchi wake kwa msaada wa awali uliotolewa na serikali sanjari na kuwahifadhi wahanga walioathiliwa na mvua hizo kwa kubomolewa numba zao.
Wananchi wamepewa tahadhari kuwa waangalifu kutokana na Mvua zilizoanza kunyesha maeneo mbalimbali nchini ambazo zimeanza kuleta madhara.

Thursday 13 December 2018

DC AONGOZA HAMASA YA WANANCHI KATIKA UJENZI WA SHULE


DC AONGOZA HAMASA YA WANANCHI KATIKA UJENZI WA SHULE

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando ameshiriki ujenzi wa Shule shikizi ya kijiji cha Songambeleiliyoko kata ya Kapalamsenga wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi ikiwa ni jitihada za wananchi wa kijiji hicho kuharakisha upatikanaji wa huduma ya elimu kijijini hapo.

Akiwa katika kijiji hicho Mkuu wa Wilaya Mhando ameshiriki katika zoezi la kusafisha eneo la ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji na Kata pamoja na wananchi kwa ujumla, kusafisha eneo hilo kisha kulipima mahali madarasa yatakapo kaa wakiongozwa na Mhandisi wa ujenzi wa Wilaya  Salum
Mkuu wa Wilaya amesema ili kurejesha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo  yao kuelekea uchumi wa  Katina viwanda ofisi yake imeamua kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa sera na ilani  kwa vitendo katika ngazi ya  jamii kushiriki na kuchangia shughuli za maendeleo yao kwa kufanya kazi bega kwa  bega na wananchi kwa kuchangia nguvu zao,rasilimali fedha, rasilimali vifaa na ufundi kwenye utekelezaji wa ujenzi wa miundo mbinu ya  elimu,afya,kilimo,mifugo, barabara na viwanda vidogovidogo.


Amesema mradi huu wa ujenzi wa shule ya  kijiji cha Songambele utasaidia kusogeza huduma ya elimu jirani na wananchi na amevutiwa na hamasa kubwa ya maendeleo ndiyo maana ameamua kushiriki na wananchi katika kuendeleza ujenzi wa madrasa ambayo  yatasaidia sana katika kutoa elimu kwa watoto wa kijiji hiki na vitongoji vyake.
Kwa upande wao wananchi nao wameahidi kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo kwa wakati ili shule zinapofunguliwa wawe na sehemu ya kusomea.

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando akishiriki katika shughuli za ujenzi wa shule kwa kufyeka eneo la ujenzi wa vyumba vya madarasa shule shikizi ya songambele Kijiji cha songambele Kata ya Kapalamsenga.
Mkuu wa Wilaya ya  Tanganyika Salehe Mhando aliyeshika jembe akiwa na wananchi na watalaamu wa Wilaya wakiweka alama kuonesha eneo la uchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule ya shikizi ya Songambele.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando mwenye kofia ya blue akishiriki na wananchi wa Kijiji cha Songambele katika shughuli za maendeleo ya kufyeka eneo la ujenzi wa shule.

Matukio mbalimbali katika picha ushiriki wa mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando katika shughuli za maendeleo kijiji cha songambele kata ya Kapalamsenga akishirikiana na wananchi kuwatia moyo kujitolea kuleta maendeleo.


Matukio mbalimbali katika picha ushiriki wa mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando katika shughuli za maendeleo kijiji cha songambele kata ya Kapalamsenga akishirikiana na wananchi kuwatia moyo kujitolea kuleta maendeleo.
Mwandishi wa Habari wa gazeti la majira mkoa wa Katavi George Mwigulu akishirikia kuchimba msingi wa ujenziwa shule ya kijiji pamoja na wananchi wa kijiji cha songambele ikiwa ni kuunga juhudi za wananchi kujiletea maendeleo kwa njia ya kujitolea.

Matukio mbalimbali katika picha ushiriki wa mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando katika shughuli za maendeleo kijiji cha songambele kata ya Kapalamsenga akishirikiana na wananchi kuwatia moyo kujitolea kuleta maendeleo.


Matukio mbalimbali katika picha ushiriki wa mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando katika shughuli za maendeleo kijiji cha songambele kata ya Kapalamsenga akishirikiana na wananchi kuwatia moyo kujitolea kuleta maendeleo.


Picha zote kitengo cha Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.









Wednesday 12 December 2018

Mpanda DC kumiliki Tongwe Magharibi