Wednesday 12 July 2017

MAONESHO YA 23 YA NANENANE NA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA


MAONESHO YA 23 YA NANENANE NA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA

Maoesho ya kilimo Nanenane kwa kanda ya nyanda za juu kusini yameingia siku ya nne huku banda la Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda likionesha kuwa na mvuto wa hali ya juu kuwafanya wananchi wengi kuvutika kuja kutembelea na kujifunza mambo yanayopatikana katika Halmashauri hiyo.
Moja ya kivutio kikubwa ni kutangaza eneo la uwekezaji la Luhafwe kama ilivyo sera ya nchi ya Viwanda ili kukuza uchumi na kuwaletea wananchi maisha mazuri kwa kutumia kilimo chenye tija. Pichani ni Afisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda akitoa maelezo na elimu ya ramani ya eneo la uwekezaji la Luhafwe kwa wananchi waliopata fursa ya kutembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda akiwemo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpanda Romuli Rojas John
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda amepongeza kwa dhati kazi nzuri inayofanyika na kuwatia moyo wananchi wa wilaya ya Tanganyika kutokana na juhudi kubwa ya kuleta maendeleo kupitia shughuli za uzalishaji hasa kilimo kwa kuwa ndiyo uti wa mgongo kwa taifa, Pia akaahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu katika kusukuma kilimo kwenye Halmashauri yake kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeeo na kusisitiza wawekezaji kuja kuwekeza kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kupitia maonesho hayo wanakaribishwa.