Wednesday 23 May 2018

Halmashauri ya wilaya ya Mpanda imekabidhiwa magari 2 na kumpyuta 25 kutoka serikali Kuu.

Halmashauri ya wilaya ya Mpanda imekabidhiwa magari 2 na kumpyuta 25 kutoka serikali Kuu. Vitendea kazi hivyo vimekabidhiwa na mbunge wa Mpanda vijijini mhe. Moshi Kakoso Mei 19, 2018 katika viwanja vya shule ya msingi Mpandandogo.
Gari moja aina ya ‘Toyota landcruiser-picup’ iliyotolewa na wizara ya maliasili na utalii kwa lengo la kulinda misitu na vyanzo vya maji katika Halmashauri ya wilaya ya Mpanda. Gari nyingine ni la kubebea wagonjwa lililotolewa na wizara ya afya, wazee, jinsia na watoto.
Hata hivyo katika hafla hiyo, Mkuu wa uendeshaji mfuko wa mawasiliano kwa wote(UCSAF) mhandisi Albert Richard amekabidi kompyuta 25 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda zenye thamani ya shilingi milioni 50. Baada ya kupokea kompyuta hizo zikakabidhiwa kwa wakuu wa shule za sekondari na moja kwenda kituo cha polisi Mishamo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Romuli Rojas John alishukuru kwa kupata magari hayo 2 na kompyuta 25. Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ina eneo kubwa kiutawala na maeneo mengi hayafikiki kiurahisi, kunahitajika magari mapya na yenye uwezo wa kuhimili changamoto za barabara zetu.
“Kwa mkoa wa Katavi, Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ndiyo halmashauri yenye eneo kubwa kuliko Halmashauri zingine. Nusu ya eneo la Halmashauri ni misitu tengefu na ushoroba. Nina watendaji vijana na wasomi wenyeuwezo wa kutunza vizuri vitendea kazi hivi.” Alisema Romuli
Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ina magari mengi makukuu na baadhi yameegeshwa kutokana na kuhitaji matengenezo makubwa na kwa gharama kubwa. Kwa mwaka wa fedha 2017/2018 tumepata magari mapya 3.


No comments:

Post a Comment