Friday 14 December 2018

ZAIDI YA NYUMBA KUMI ZIMEATHIRIKA KUTOKANA NA MVUA


ZAIDI YA NYUMBA KUMI ZIMEATHIRIKA KUTOKANA NA MVUA

Zaidi ya nyumba kumi zimeathirika kutokana na mvua iliyonyesha juzi ikiwa imeambatana na upepo mkali katika kijiji cha kabungu Kata ya Kabungu Wilaya ya Tanganyika na kusabaisha familia nane kukosa makazi na kuhifadhiwa na wasamalia wema.


Akitoa taarifa  ya athari za mvua hiyo mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya iliyoongoza na kamati kamati ya maafa Afisa taarafa wa Tarafa ya Kabungu Odes Gwamaka ameleza kuwa baada ya kupokea taarifa hizo uongozi wa serikali ya kijiji kata na Tarafa walifika eneo la tukio kuwajulia hali wahanga na  kuchukua hatua za haraka kuwapa msaada wa kibinadamu ikiwa ni pamoja na kuwatafutia mahali pa kulala kwa wale walioezuliwa nyumba zao.
 Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama na kamati ya maafa ya wilaya ametembelea  wahanga na kuwapa pole na msaada ya awali ya kibinadamu kama chakula,na kutoa maaelekzeo tathimini ifanyike mapema ili kujua hasara iliyopatikana 

Aidha amewaelekeza wananchi wanapojenga nyumba waepuke ile tabia iliyozoelekea ya kutokufunga lenta ,kwani nyumba yenye lenta inakuwa imara Zaidi,na kusisitiza kupanda miti kwenye maeneo yao kwa kuwa inasaidia kupunguza kasi ya upepo  pindi mvua zinaponyesha zhasa zile za upepo mkali.   

 Kwa Upande wake Katibu wa Kamati ya maafa ya  wilaya ya Tanganyika Reginald Mhango ambaye pia ni Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya  kwa kushirikiana na uongozi wa Kijiji ,Kata  na Tarafa  ametoa mchanganua wa msaada uliopatikana  na jinsi utukagawiwa kwa walengwa,ambapo kwa harakahara vitu vilivyolewa unga wa sembe,maharage,sabuni sukari vinathamani ya Zaidi ya shilingi laki tano kwa kuthamanisha.

Diwani wa Kata ya Kabungu Christina Reonard Sanane ameshukuru kwa niaba ya wananchi wake kwa msaada wa awali uliotolewa na serikali sanjari na kuwahifadhi wahanga walioathiliwa na mvua hizo kwa kubomolewa numba zao.
Wananchi wamepewa tahadhari kuwa waangalifu kutokana na Mvua zilizoanza kunyesha maeneo mbalimbali nchini ambazo zimeanza kuleta madhara.

No comments:

Post a Comment