DC
AONGOZA HAMASA YA WANANCHI KATIKA UJENZI WA SHULE
Mkuu wa
Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando ameshiriki ujenzi wa Shule shikizi ya kijiji
cha Songambeleiliyoko kata ya Kapalamsenga wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi
ikiwa ni jitihada za wananchi wa kijiji hicho kuharakisha upatikanaji wa huduma
ya elimu kijijini hapo.
Akiwa
katika kijiji hicho Mkuu wa Wilaya Mhando ameshiriki katika zoezi la kusafisha
eneo la ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji na
Kata pamoja na wananchi kwa ujumla, kusafisha eneo hilo kisha kulipima mahali
madarasa yatakapo kaa wakiongozwa na Mhandisi wa ujenzi wa Wilaya Salum
Mkuu wa Wilaya amesema ili kurejesha ari ya
wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo
yao kuelekea uchumi wa Katina viwanda
ofisi yake imeamua kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa sera na ilani kwa vitendo katika ngazi ya jamii kushiriki na kuchangia shughuli za
maendeleo yao kwa kufanya kazi bega kwa
bega na wananchi kwa kuchangia nguvu zao,rasilimali fedha, rasilimali
vifaa na ufundi kwenye utekelezaji wa ujenzi wa miundo mbinu ya elimu,afya,kilimo,mifugo, barabara na viwanda
vidogovidogo.

Amesema
mradi huu wa ujenzi wa shule ya kijiji
cha Songambele utasaidia kusogeza huduma ya elimu jirani na wananchi na
amevutiwa na hamasa kubwa ya maendeleo ndiyo maana ameamua kushiriki na
wananchi katika kuendeleza ujenzi wa madrasa ambayo yatasaidia sana katika kutoa elimu kwa watoto
wa kijiji hiki na vitongoji vyake.
Kwa
upande wao wananchi nao wameahidi kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo kwa
wakati ili shule zinapofunguliwa wawe na sehemu ya kusomea.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika
Salehe Mhando akishiriki katika shughuli za ujenzi wa shule kwa kufyeka eneo la
ujenzi wa vyumba vya madarasa shule shikizi ya songambele Kijiji cha songambele
Kata ya Kapalamsenga.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando aliyeshika jembe
akiwa na wananchi na watalaamu wa Wilaya wakiweka alama kuonesha eneo la
uchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule ya shikizi
ya Songambele.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika
Salehe Mhando mwenye kofia ya blue akishiriki na wananchi wa Kijiji cha
Songambele katika shughuli za maendeleo ya kufyeka eneo la ujenzi wa shule.
Matukio mbalimbali katika picha
ushiriki wa mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando katika shughuli za
maendeleo kijiji cha songambele kata ya Kapalamsenga akishirikiana na wananchi
kuwatia moyo kujitolea kuleta maendeleo.

Mwandishi wa Habari wa gazeti la
majira mkoa wa Katavi George Mwigulu akishirikia kuchimba msingi wa ujenziwa
shule ya kijiji pamoja na wananchi wa kijiji cha songambele ikiwa ni kuunga
juhudi za wananchi kujiletea maendeleo kwa njia ya kujitolea.
Matukio mbalimbali katika picha
ushiriki wa mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando katika shughuli za
maendeleo kijiji cha songambele kata ya Kapalamsenga akishirikiana na wananchi
kuwatia moyo kujitolea kuleta maendeleo.
Matukio mbalimbali katika picha
ushiriki wa mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando katika shughuli za
maendeleo kijiji cha songambele kata ya Kapalamsenga akishirikiana na wananchi
kuwatia moyo kujitolea kuleta maendeleo.
Picha zote
kitengo cha Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
No comments:
Post a Comment