Thursday, 20 December 2018
Friday, 14 December 2018
ZAIDI YA NYUMBA KUMI ZIMEATHIRIKA KUTOKANA NA MVUA
ZAIDI YA NYUMBA KUMI ZIMEATHIRIKA KUTOKANA NA MVUA
Zaidi ya nyumba kumi zimeathirika kutokana na mvua
iliyonyesha juzi ikiwa imeambatana na upepo mkali katika kijiji cha kabungu
Kata ya Kabungu Wilaya ya Tanganyika na kusabaisha familia nane kukosa makazi
na kuhifadhiwa na wasamalia wema.
Akitoa taarifa ya
athari za mvua hiyo mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya iliyoongoza
na kamati kamati ya maafa Afisa taarafa wa Tarafa ya Kabungu Odes Gwamaka
ameleza kuwa baada ya kupokea taarifa hizo uongozi wa serikali ya kijiji kata
na Tarafa walifika eneo la tukio kuwajulia hali wahanga na kuchukua hatua za haraka kuwapa msaada wa
kibinadamu ikiwa ni pamoja na kuwatafutia mahali pa kulala kwa wale
walioezuliwa nyumba zao.
Mkuu wa Wilaya ya
Tanganyika Salehe Mhando ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
usalama na kamati ya maafa ya wilaya ametembelea wahanga na kuwapa pole na msaada ya awali ya
kibinadamu kama chakula,na kutoa maaelekzeo tathimini ifanyike mapema ili kujua
hasara iliyopatikana
Aidha amewaelekeza wananchi wanapojenga nyumba waepuke ile
tabia iliyozoelekea ya kutokufunga lenta ,kwani nyumba yenye lenta inakuwa
imara Zaidi,na kusisitiza kupanda miti kwenye maeneo yao kwa kuwa inasaidia
kupunguza kasi ya upepo pindi mvua
zinaponyesha zhasa zile za upepo mkali.
Kwa Upande wake Katibu
wa Kamati ya maafa ya wilaya ya Tanganyika
Reginald Mhango ambaye pia ni Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya kwa kushirikiana na uongozi wa Kijiji
,Kata na Tarafa ametoa mchanganua wa msaada uliopatikana na jinsi utukagawiwa kwa walengwa,ambapo kwa
harakahara vitu vilivyolewa unga wa sembe,maharage,sabuni sukari vinathamani ya
Zaidi ya shilingi laki tano kwa kuthamanisha.
Diwani wa Kata ya Kabungu Christina Reonard Sanane
ameshukuru kwa niaba ya wananchi wake kwa msaada wa awali uliotolewa na
serikali sanjari na kuwahifadhi wahanga walioathiliwa na mvua hizo kwa
kubomolewa numba zao.
Wananchi wamepewa tahadhari kuwa waangalifu kutokana na Mvua
zilizoanza kunyesha maeneo mbalimbali nchini ambazo zimeanza kuleta madhara.
Thursday, 13 December 2018
DC AONGOZA HAMASA YA WANANCHI KATIKA UJENZI WA SHULE
DC
AONGOZA HAMASA YA WANANCHI KATIKA UJENZI WA SHULE
Mkuu wa
Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando ameshiriki ujenzi wa Shule shikizi ya kijiji
cha Songambeleiliyoko kata ya Kapalamsenga wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi
ikiwa ni jitihada za wananchi wa kijiji hicho kuharakisha upatikanaji wa huduma
ya elimu kijijini hapo.
Akiwa
katika kijiji hicho Mkuu wa Wilaya Mhando ameshiriki katika zoezi la kusafisha
eneo la ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji na
Kata pamoja na wananchi kwa ujumla, kusafisha eneo hilo kisha kulipima mahali
madarasa yatakapo kaa wakiongozwa na Mhandisi wa ujenzi wa Wilaya Salum
Mkuu wa Wilaya amesema ili kurejesha ari ya
wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo
yao kuelekea uchumi wa Katina viwanda
ofisi yake imeamua kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa sera na ilani kwa vitendo katika ngazi ya jamii kushiriki na kuchangia shughuli za
maendeleo yao kwa kufanya kazi bega kwa
bega na wananchi kwa kuchangia nguvu zao,rasilimali fedha, rasilimali
vifaa na ufundi kwenye utekelezaji wa ujenzi wa miundo mbinu ya elimu,afya,kilimo,mifugo, barabara na viwanda
vidogovidogo.

Amesema
mradi huu wa ujenzi wa shule ya kijiji
cha Songambele utasaidia kusogeza huduma ya elimu jirani na wananchi na
amevutiwa na hamasa kubwa ya maendeleo ndiyo maana ameamua kushiriki na
wananchi katika kuendeleza ujenzi wa madrasa ambayo yatasaidia sana katika kutoa elimu kwa watoto
wa kijiji hiki na vitongoji vyake.
Kwa
upande wao wananchi nao wameahidi kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo kwa
wakati ili shule zinapofunguliwa wawe na sehemu ya kusomea.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika
Salehe Mhando akishiriki katika shughuli za ujenzi wa shule kwa kufyeka eneo la
ujenzi wa vyumba vya madarasa shule shikizi ya songambele Kijiji cha songambele
Kata ya Kapalamsenga.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando aliyeshika jembe
akiwa na wananchi na watalaamu wa Wilaya wakiweka alama kuonesha eneo la
uchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule ya shikizi
ya Songambele.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika
Salehe Mhando mwenye kofia ya blue akishiriki na wananchi wa Kijiji cha
Songambele katika shughuli za maendeleo ya kufyeka eneo la ujenzi wa shule.
Matukio mbalimbali katika picha
ushiriki wa mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando katika shughuli za
maendeleo kijiji cha songambele kata ya Kapalamsenga akishirikiana na wananchi
kuwatia moyo kujitolea kuleta maendeleo.
Matukio mbalimbali katika picha
ushiriki wa mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando katika shughuli za
maendeleo kijiji cha songambele kata ya Kapalamsenga akishirikiana na wananchi
kuwatia moyo kujitolea kuleta maendeleo.
Mwandishi wa Habari wa gazeti la
majira mkoa wa Katavi George Mwigulu akishirikia kuchimba msingi wa ujenziwa
shule ya kijiji pamoja na wananchi wa kijiji cha songambele ikiwa ni kuunga
juhudi za wananchi kujiletea maendeleo kwa njia ya kujitolea.
Matukio mbalimbali katika picha
ushiriki wa mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando katika shughuli za
maendeleo kijiji cha songambele kata ya Kapalamsenga akishirikiana na wananchi
kuwatia moyo kujitolea kuleta maendeleo.
Matukio mbalimbali katika picha
ushiriki wa mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando katika shughuli za
maendeleo kijiji cha songambele kata ya Kapalamsenga akishirikiana na wananchi
kuwatia moyo kujitolea kuleta maendeleo.
Picha zote
kitengo cha Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
Wednesday, 12 December 2018
Mpanda DC kumiliki Tongwe Magharibi
Mpanda DC kumiliki Tongwe Magharibi
WANANCHI WA VIJIJI VYA MSITU TOGWE WATABASAM
Wananchi wa vijiji vinavyozungwa na msitu wa Tongwe Magharibi
wameanza kufurahia baada ya kusikia waziri wa maliasili na utalii Mhe.
Hamis Kigwangalla amesaini kusudio la kumilikisha msitu huo kwa
Halmashauri ya wilaya ya Mpanda. Msitu huo wenye ukubwa wa zaidi ya
hekta 330,000 umezungukwa na vijiji 15 na elimu ya kuwaelimisha na
kupokea maoni ya wananchi kwa awamu ya pili imeanza mwishoni mwa
Novemba, 2018 na itaendele hadi mwanzoni mwa januari 2019.
Furaha ya wananchi ilionekana mara tu baada ya kaimu Mkuu wa idara ya
ardhi na maliasili Bw. Elisha Mengele kuwaeleza kwenye mikutano ya
hadhara inayoendelea katika vijiji hivyo vinavyozungukwa na msitu wa
Tongwe Magharibi.
“Ndugu wananchi mnakukumbuka kuwa mwanzoni mwa mwezi wa sita timu
ya viongozi wa wilaya ya Tanganyika, Halmashauri ya wilaya ya Mpanda na
uongozi wa chama na serikali wa wilaya ya Tanganyika walifika
kuwaelimisha faida za msitu wa Tongwe Magharibi kwa wananchi endapo
msitu huo utamilikiwa na Halmashauri ya wilaya ya Mpanda”. Alifafanua Elisha Mengele.
Aidha, faida zitokanazo na msitu huo wa Tongwe Magharibi ni pamoja na
chazo cha kudumu cha mito zaidi 16, ajira kwa vijana 6 kwa kila kijiji
kilichozungukwa na msitu huo, uvunaji wa hewa ya ukaa na ufugaji wa
nyuki. Faida zingine ni pamoja na shughuli za kiutalii kwani ndani yam
situ huo kuna sokwe wa kutosha.
Subscribe to:
Posts (Atom)