Mpanda DC kumiliki Tongwe Magharibi
WANANCHI WA VIJIJI VYA MSITU TOGWE WATABASAM
Wananchi wa vijiji vinavyozungwa na msitu wa Tongwe Magharibi
wameanza kufurahia baada ya kusikia waziri wa maliasili na utalii Mhe.
Hamis Kigwangalla amesaini kusudio la kumilikisha msitu huo kwa
Halmashauri ya wilaya ya Mpanda. Msitu huo wenye ukubwa wa zaidi ya
hekta 330,000 umezungukwa na vijiji 15 na elimu ya kuwaelimisha na
kupokea maoni ya wananchi kwa awamu ya pili imeanza mwishoni mwa
Novemba, 2018 na itaendele hadi mwanzoni mwa januari 2019.
Furaha ya wananchi ilionekana mara tu baada ya kaimu Mkuu wa idara ya
ardhi na maliasili Bw. Elisha Mengele kuwaeleza kwenye mikutano ya
hadhara inayoendelea katika vijiji hivyo vinavyozungukwa na msitu wa
Tongwe Magharibi.
“Ndugu wananchi mnakukumbuka kuwa mwanzoni mwa mwezi wa sita timu
ya viongozi wa wilaya ya Tanganyika, Halmashauri ya wilaya ya Mpanda na
uongozi wa chama na serikali wa wilaya ya Tanganyika walifika
kuwaelimisha faida za msitu wa Tongwe Magharibi kwa wananchi endapo
msitu huo utamilikiwa na Halmashauri ya wilaya ya Mpanda”. Alifafanua Elisha Mengele.
Aidha, faida zitokanazo na msitu huo wa Tongwe Magharibi ni pamoja na
chazo cha kudumu cha mito zaidi 16, ajira kwa vijana 6 kwa kila kijiji
kilichozungukwa na msitu huo, uvunaji wa hewa ya ukaa na ufugaji wa
nyuki. Faida zingine ni pamoja na shughuli za kiutalii kwani ndani yam
situ huo kuna sokwe wa kutosha.
No comments:
Post a Comment