Thursday, 11 April 2019
Saturday, 9 March 2019
HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA YATIKISA KATIKA UINGIZAJI WA TAARIFA ZA SHULE
SEMINA YA MAFUNZO YA VISHIKWAMBI HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA
Walimu wa Shule za Msing Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda wakisikiliza mafunzo ya namana ya kutumia kishikwambi (tablet). walimu hao wamewezeshawa kutumia taarifa muhimu kutoka shule walizopo moja kwa moja kupitia vishikwambi walivyopewa kwa matumizi ya kutunza taarifa za shule zao.Mafunzo hayo ya siku nne yaliyofadhiliwa kupitia programu ya EQUIP Tanzania yalianza tarehe 4/03/2019 na yatakamilika 8/03/2019
Friday, 1 February 2019
HALMASHAURI YA WILAYA YA MPNDA YAJIPANGA KIKAMILIFU KUIMARISHA MBINU ZA UFUNDISHAJI MASHULENI.
HALMASHAURI YA WILAYA YA MPNDA YAJIPANGA KIKAMILIFU KUIMARISHA MBINU ZA UFUNDISHAJI MASHULENI.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda (wa kwanza kutoka kulia) akiongozana na afisa elimu msingi Bw. Kenny Shilumba na sisita Rose Sungura wakiangalia zana za kufundishia wanafunzi wa awali na darasa la kwanza. Mafunzo hayo yameratibiwa na OR-TAMISEMI kwa kushirikiana EQUIP- Tanzania. Jumla ya walimu 82 na maafisa elimu wa kata 13 wamepatiwa mafunzo ya namna ya kuinua elimu katika wilaya ya Tanganyika.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda (wa kwanza kutoka kulia) akiongozana na afisa elimu msingi Bw. Kenny Shilumba na sisita Rose Sungura wakiangalia zana za kufundishia wanafunzi wa awali na darasa la kwanza. Mafunzo hayo yameratibiwa na OR-TAMISEMI kwa kushirikiana EQUIP- Tanzania. Jumla ya walimu 82 na maafisa elimu wa kata 13 wamepatiwa mafunzo ya namna ya kuinua elimu katika wilaya ya Tanganyika.
NIMWENDO WA JET KWENYE UJENZI WA MADARASA
HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA NIMWENDO WA JET KWENYE UJENZI WA MADARASA
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Bw. Romuli Rojas John (wa kwanza kutoka kulia) akiwa na afisa mipango Bw. Dotto Kwigena na Afisa elimu sekondari Bw. Michael Lyambilo, wakiteta jambo katika eneo la ujenzi wa sekondari Sibwesa. Siku hiyo uongozi wa mkoa wa Katavi na wilaya ya Tanganyika walifika kuona hatua ya ujenzi wa shule mpya ili ziweze kufunguliwa na kuchukua wanafunzi 2019.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Bw. Romuli Rojas John (wa kwanza kutoka kulia) akiwa na afisa mipango Bw. Dotto Kwigena na Afisa elimu sekondari Bw. Michael Lyambilo, wakiteta jambo katika eneo la ujenzi wa sekondari Sibwesa. Siku hiyo uongozi wa mkoa wa Katavi na wilaya ya Tanganyika walifika kuona hatua ya ujenzi wa shule mpya ili ziweze kufunguliwa na kuchukua wanafunzi 2019.
HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA YA JIPANGA KIKAMILIFU JUU YA DARASA LA AWALI
HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA YA JIPANGA KIKAMILIFU JUU YA DARASA LA AWALI
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Bw. Romuli Rojas John (wa kwanza kutoka kulia) akiangalia moja ya zana ya ufundishaji iliyotengenezwa na mwali wa darasa la kwanza. Zana hiyo imetengenezwa kwa kutumia mmea wa upupu pamoja na karatasi ya manila
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Bw. Romuli Rojas John (wa kwanza kutoka kulia) akiangalia moja ya zana ya ufundishaji iliyotengenezwa na mwali wa darasa la kwanza. Zana hiyo imetengenezwa kwa kutumia mmea wa upupu pamoja na karatasi ya manila
MPAKA KIELEWEKE
HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA YA JIPANGA KIKAMILIFU JUU YA DARASA LA AWALI "MPAKA KIELEWEKE"
Hiki ni mfano wa kitanda kilichoandaliwa na mwalimu wa madarasa ya awali na kwanza kwa ajili ya kufundishia watoto namna ya kuandaa kitanda kabla ya kulala. Mambo kama haya yanasaidia kuwafundisha watoto wawe nadhifu na kutunza miili yao na kuwa safi muda wote. Mafunzo hayo yamefanyika Januari 28, 2019 katika ukumbi wa shule ya Mt. Maria-Mpanda.
Hiki ni mfano wa kitanda kilichoandaliwa na mwalimu wa madarasa ya awali na kwanza kwa ajili ya kufundishia watoto namna ya kuandaa kitanda kabla ya kulala. Mambo kama haya yanasaidia kuwafundisha watoto wawe nadhifu na kutunza miili yao na kuwa safi muda wote. Mafunzo hayo yamefanyika Januari 28, 2019 katika ukumbi wa shule ya Mt. Maria-Mpanda.
Bw. Amosi Makala atiatimu Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda
Mkuu wa mkoa wa Katavi Bw. Amosi Makalla (wa pili kutoka kushoto)
amefanya ziara ya kutembelea shule za sekondari zinazotarajia kuchukua
wanafunzi waliofauli na kukosa nafasi. Wilayani Tanganyika kuna
wanafunzi 363 na wanatarajia kujiunga kidato cha kwanza 2019 katika
shule za Sibwesa, Bulamata na Ilangu.
Wednesday, 16 January 2019
TANGAZO LA KUITWA KAZINI HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA
MAJINA MENGINE YANAPATIKANA KWENYE TOVUTI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA
Bofya hapa kupata taarifa.Tangazo la kitwa kazini MpandaDC.jpg
Thursday, 20 December 2018
NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA
Friday, 14 December 2018
ZAIDI YA NYUMBA KUMI ZIMEATHIRIKA KUTOKANA NA MVUA
ZAIDI YA NYUMBA KUMI ZIMEATHIRIKA KUTOKANA NA MVUA
Zaidi ya nyumba kumi zimeathirika kutokana na mvua
iliyonyesha juzi ikiwa imeambatana na upepo mkali katika kijiji cha kabungu
Kata ya Kabungu Wilaya ya Tanganyika na kusabaisha familia nane kukosa makazi
na kuhifadhiwa na wasamalia wema.
Akitoa taarifa ya
athari za mvua hiyo mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya iliyoongoza
na kamati kamati ya maafa Afisa taarafa wa Tarafa ya Kabungu Odes Gwamaka
ameleza kuwa baada ya kupokea taarifa hizo uongozi wa serikali ya kijiji kata
na Tarafa walifika eneo la tukio kuwajulia hali wahanga na kuchukua hatua za haraka kuwapa msaada wa
kibinadamu ikiwa ni pamoja na kuwatafutia mahali pa kulala kwa wale
walioezuliwa nyumba zao.
Mkuu wa Wilaya ya
Tanganyika Salehe Mhando ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
usalama na kamati ya maafa ya wilaya ametembelea wahanga na kuwapa pole na msaada ya awali ya
kibinadamu kama chakula,na kutoa maaelekzeo tathimini ifanyike mapema ili kujua
hasara iliyopatikana
Aidha amewaelekeza wananchi wanapojenga nyumba waepuke ile
tabia iliyozoelekea ya kutokufunga lenta ,kwani nyumba yenye lenta inakuwa
imara Zaidi,na kusisitiza kupanda miti kwenye maeneo yao kwa kuwa inasaidia
kupunguza kasi ya upepo pindi mvua
zinaponyesha zhasa zile za upepo mkali.
Kwa Upande wake Katibu
wa Kamati ya maafa ya wilaya ya Tanganyika
Reginald Mhango ambaye pia ni Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya kwa kushirikiana na uongozi wa Kijiji
,Kata na Tarafa ametoa mchanganua wa msaada uliopatikana na jinsi utukagawiwa kwa walengwa,ambapo kwa
harakahara vitu vilivyolewa unga wa sembe,maharage,sabuni sukari vinathamani ya
Zaidi ya shilingi laki tano kwa kuthamanisha.
Diwani wa Kata ya Kabungu Christina Reonard Sanane
ameshukuru kwa niaba ya wananchi wake kwa msaada wa awali uliotolewa na
serikali sanjari na kuwahifadhi wahanga walioathiliwa na mvua hizo kwa
kubomolewa numba zao.
Wananchi wamepewa tahadhari kuwa waangalifu kutokana na Mvua
zilizoanza kunyesha maeneo mbalimbali nchini ambazo zimeanza kuleta madhara.
Thursday, 13 December 2018
DC AONGOZA HAMASA YA WANANCHI KATIKA UJENZI WA SHULE
DC
AONGOZA HAMASA YA WANANCHI KATIKA UJENZI WA SHULE
Mkuu wa
Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando ameshiriki ujenzi wa Shule shikizi ya kijiji
cha Songambeleiliyoko kata ya Kapalamsenga wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi
ikiwa ni jitihada za wananchi wa kijiji hicho kuharakisha upatikanaji wa huduma
ya elimu kijijini hapo.
Akiwa
katika kijiji hicho Mkuu wa Wilaya Mhando ameshiriki katika zoezi la kusafisha
eneo la ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji na
Kata pamoja na wananchi kwa ujumla, kusafisha eneo hilo kisha kulipima mahali
madarasa yatakapo kaa wakiongozwa na Mhandisi wa ujenzi wa Wilaya Salum
Mkuu wa Wilaya amesema ili kurejesha ari ya
wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo
yao kuelekea uchumi wa Katina viwanda
ofisi yake imeamua kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa sera na ilani kwa vitendo katika ngazi ya jamii kushiriki na kuchangia shughuli za
maendeleo yao kwa kufanya kazi bega kwa
bega na wananchi kwa kuchangia nguvu zao,rasilimali fedha, rasilimali
vifaa na ufundi kwenye utekelezaji wa ujenzi wa miundo mbinu ya elimu,afya,kilimo,mifugo, barabara na viwanda
vidogovidogo.

Amesema
mradi huu wa ujenzi wa shule ya kijiji
cha Songambele utasaidia kusogeza huduma ya elimu jirani na wananchi na
amevutiwa na hamasa kubwa ya maendeleo ndiyo maana ameamua kushiriki na
wananchi katika kuendeleza ujenzi wa madrasa ambayo yatasaidia sana katika kutoa elimu kwa watoto
wa kijiji hiki na vitongoji vyake.
Kwa
upande wao wananchi nao wameahidi kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo kwa
wakati ili shule zinapofunguliwa wawe na sehemu ya kusomea.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika
Salehe Mhando akishiriki katika shughuli za ujenzi wa shule kwa kufyeka eneo la
ujenzi wa vyumba vya madarasa shule shikizi ya songambele Kijiji cha songambele
Kata ya Kapalamsenga.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando aliyeshika jembe
akiwa na wananchi na watalaamu wa Wilaya wakiweka alama kuonesha eneo la
uchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule ya shikizi
ya Songambele.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika
Salehe Mhando mwenye kofia ya blue akishiriki na wananchi wa Kijiji cha
Songambele katika shughuli za maendeleo ya kufyeka eneo la ujenzi wa shule.
Matukio mbalimbali katika picha
ushiriki wa mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando katika shughuli za
maendeleo kijiji cha songambele kata ya Kapalamsenga akishirikiana na wananchi
kuwatia moyo kujitolea kuleta maendeleo.
Matukio mbalimbali katika picha
ushiriki wa mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando katika shughuli za
maendeleo kijiji cha songambele kata ya Kapalamsenga akishirikiana na wananchi
kuwatia moyo kujitolea kuleta maendeleo.
Mwandishi wa Habari wa gazeti la
majira mkoa wa Katavi George Mwigulu akishirikia kuchimba msingi wa ujenziwa
shule ya kijiji pamoja na wananchi wa kijiji cha songambele ikiwa ni kuunga
juhudi za wananchi kujiletea maendeleo kwa njia ya kujitolea.
Matukio mbalimbali katika picha
ushiriki wa mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando katika shughuli za
maendeleo kijiji cha songambele kata ya Kapalamsenga akishirikiana na wananchi
kuwatia moyo kujitolea kuleta maendeleo.
Matukio mbalimbali katika picha
ushiriki wa mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando katika shughuli za
maendeleo kijiji cha songambele kata ya Kapalamsenga akishirikiana na wananchi
kuwatia moyo kujitolea kuleta maendeleo.
Picha zote
kitengo cha Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
Wednesday, 12 December 2018
Mpanda DC kumiliki Tongwe Magharibi
Mpanda DC kumiliki Tongwe Magharibi
WANANCHI WA VIJIJI VYA MSITU TOGWE WATABASAM
Wananchi wa vijiji vinavyozungwa na msitu wa Tongwe Magharibi
wameanza kufurahia baada ya kusikia waziri wa maliasili na utalii Mhe.
Hamis Kigwangalla amesaini kusudio la kumilikisha msitu huo kwa
Halmashauri ya wilaya ya Mpanda. Msitu huo wenye ukubwa wa zaidi ya
hekta 330,000 umezungukwa na vijiji 15 na elimu ya kuwaelimisha na
kupokea maoni ya wananchi kwa awamu ya pili imeanza mwishoni mwa
Novemba, 2018 na itaendele hadi mwanzoni mwa januari 2019.
Furaha ya wananchi ilionekana mara tu baada ya kaimu Mkuu wa idara ya
ardhi na maliasili Bw. Elisha Mengele kuwaeleza kwenye mikutano ya
hadhara inayoendelea katika vijiji hivyo vinavyozungukwa na msitu wa
Tongwe Magharibi.
“Ndugu wananchi mnakukumbuka kuwa mwanzoni mwa mwezi wa sita timu
ya viongozi wa wilaya ya Tanganyika, Halmashauri ya wilaya ya Mpanda na
uongozi wa chama na serikali wa wilaya ya Tanganyika walifika
kuwaelimisha faida za msitu wa Tongwe Magharibi kwa wananchi endapo
msitu huo utamilikiwa na Halmashauri ya wilaya ya Mpanda”. Alifafanua Elisha Mengele.
Aidha, faida zitokanazo na msitu huo wa Tongwe Magharibi ni pamoja na
chazo cha kudumu cha mito zaidi 16, ajira kwa vijana 6 kwa kila kijiji
kilichozungukwa na msitu huo, uvunaji wa hewa ya ukaa na ufugaji wa
nyuki. Faida zingine ni pamoja na shughuli za kiutalii kwani ndani yam
situ huo kuna sokwe wa kutosha.
Wednesday, 17 October 2018
SERIKALI HAITAMWONEA AIBU ASIYELIPA KODI YA MADINI
Kibada Ernest Kibada - Katavi.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amesema kuwa Serikali kupitia
Wizara ya Madini haitamwonea aibu mchimbaji yeyote wa madini atakayekwepa
kulipa kodi Serikalini kwa kuwa ni
kinyume na Sheria ya Madini pamoja na kanuni zake.
Ameyasema hayo leo tarehe Oktoba
11, 2018 katika mkutano wake na
wachimbaji wadogo wa madini wanaoendesha shughuli zao katika machimbo ya Dirifu, yaliyopo katika kata ya Magamba mkoani
Katavi ikiwa ni sehemu ya ziara yake
katika mkoa huo yenye lengo la
kukagua shughuli za uchimbaji wa madini,
kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.
Katika ziara yake Nyongo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya
Tanganyika, Salehe Mhando, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wa Madini
Mkoa wa Katavi (KATAREMA), William Mbongo, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa
Katavi, Mhandisi Giliard Luyoka, Wataalam wa Madini, Vyombo vya Ulinzi na
Usalama pamoja na waandishi wa habari.
Alisema kuwa, kumekuwa na tabia ya baadhi ya wachimbaji wadogo wa
madini wasio waaminifu wanaokwepa kulipa kodi serikalini hali
inayokwamisha upatikanaji wa huduma
nyingine muhimu katika jamii kama vile elimu, maji, barabara.
“ Mchimbaji ambaye anakwepa kulipa kodi mbalimbali kama Sheria ya
Madini na kanuni zake inavyofafanua ni adui namba moja katika ukuaji wa
maendeleo ya nchi, hivyo sisi kama Wizara ya Madini tumejipanga kuchukua hatua
za kisheria nia ikiwa ni kutaka kila mwananchi anufaike na rasilimali za madini
kupitia uboreshaji wa huduma mbalimbali,”alisema Nyongo
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Nyongo aliwataka maafisa madini
wakazi katika mikoa yote kuwa wabunifu kwenye ukusanyaji wa maduhuli kwani
Sekta ya Madini inatarajiwa mno kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.
Aliendelea kusema kuwa, Serikali inaamini kuwa iwapo Sekta ya Madini
itasimamiwa kikamilifu, inaweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia uimarishaji
wa sekta nyingine muhimu.
Aidha, aliwataka maafisa madini nchini kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika wilaya
kwenye zoezi la ukaguzi wa shughuli za madini ili kuongeza tija kwenye ukaguzi.
Katika mkutano huo mbali na wachimbaji wadogo kumpongeza kwa kazi kubwa
anayofanya ya kusikiliza na kutatua changamoto kwenye shughuli za uchimbaji madini katika mkoa wa
Katavi, wachimbaji hao waliwasilisha changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na
mahitaji ya mikopo katika shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini, mafunzo
kuhusu sheria ya madini na kanuni zake, uchimbaji salama na vifaa vya kisasa
kwa ajili ya uchimbaji wa madini.
Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji wadogo katika eneo hilo, Imso
Masumbuko kutoka kikundi cha Kagera Group alisema kuwa wana uhitaji mkubwa wa
elimu kuhusu uchimbaji wa madini salama
pamoja na vifaa vya kisasa ili waweze kuzalisha na kulipa kodi zaidi
Serikalini.
Masumbuko mbali na kuainisha changamoto hizo
aliiomba Wizara ya Madini kuiomba Wizara ya Nishati ili iweze kufikisha umeme
katika machimbo hayo kupitia Mradi wa
Usambazaji wa Umeme Vijijini unaosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini Awamu
ya Tatu REA III
Alifafanua kuwa, kutokana na ukosefu wa nishati ya umeme katika eneo
lao wamekuwa wakitumia gharama kubwa kwenye uzalishaji wa madini kutokana na
matumizi ya dizeli hivyo kupata faida kidogo sana.
Naye Karusum Daudi ambaye ni mchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo
hilo aliiomba Serikali kupitia Wizara ya Madini iangalie uwezekano wa kuwapatia
mikopo ili waweze kuchimba kwa kutumia vifaa vya kisasa.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Nyongo alifanya ziara katika Ofisi
ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi na kusikiliza kero mbalimbali za
watumishi ikiwa ni pamoja na kuzitatua.
Pia Naibu Waziri Nyongo alikutana na wachimbaji wadogo wa madini mjini
Mpanda lengo likiwa ni kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali
zinazowakabili kwenye shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini.
Mbali na kuwasilisha changamoto mbalimbali zilizotatuliwa na Naibu
Waziri Nyongo papo hapo wachimbaji
wadogo wa madini walimpongeza Naibu Waziri Nyongo na kumwomba kuendelea na ari
ya kusikiliza kero zao na kuzitatua.
Akizungumza katika kikao hicho, Nyongo alisema Wizara ya Madini
haitachoka kutatua changamoto zinazowakabili wachimbaji wa madini nchini kwa
kuwa inataka wachimbe katika mazingira mazuri na kulipa kodi Serikalini.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza na wachimbaji
wadogo wa madini katika machimbo ya Dirifu,
yaliyopo katika kata ya Magamba mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya ziara
yake katika mkoa huo yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa
madini tarehe Oktoba 11, 2018
Sehemu ya wachimbaji wadogo wa madini kutoka machimbo ya Dirifu, yaliyopo katika kata ya Magamba mkoani
Katavi wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Naibu Waziri wa Madini
Stanslaus Nyongo (hayupo pichani kwenye mkutano wa hadhara
Mmoja wa wachimbaji wadogo wa madini katika machimbo ya Dirifu, yaliyopo katika kata ya Magamba mkoani
Katavi akiwasilisha kero yake mbele ya Naibu
Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo. (hayupo pichani)
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (katikati) akioneshwa mchoro wa
ramani ya jengo linalojengwa la Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi
na Mhandisi Andrew Mpangalala kutoka
SUMA JKT ( wa kwanza kulia) ambao ndio wajenzi wa jengo hilo katika eneo la
Msasani mjini Mpanda mkoani Katavi.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus
Nyongo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Afisa
Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi mara baada ya kufanya nao kikao kilicholenga
kujadili utendaji kazi.
(Picha zote na Kibada Ernest
Kibada wa Katavi Press Club.)
MWISHO.
Subscribe to:
Posts (Atom)







